Habari

MANCHESTER UNITED YAICHAKAZA WEST HAM 4-1 NA KUCHUNGULIA KOMBE LA EFL …Ibrahimovic, Martial moto chini, Schweinsteiger atoa gundu

on

MANCHESTER UNITED imeibuka na ushindi mnono wa 4-1 dhidi ya West Ham katika mchezo wa robo fainali ya EFL Cup iliyochezwa Old Trafford.
United itakutana na Hull City kwenye nusu fainali na iwapo itapenya basi itakuwa na kibarua kizito katika fainali itakayopigwa Wembley ambayo itawakutanisha na aidha Liverpool au Southampton.
Zlatan Ibrahimovic aliifungia United bao la kwanza katika dakika ya pili kufuatia pande zuri la Mkhitaryan ambaye kwa jana usiku alikuwa nyota wa mchezo.
Kinda wa zamani wa Manchester United Ashley Fletcher akaisawazishia West Ham kunako dakika ya 35 na kufanya timu hizo ziende mapumziko zikiwa nguvu sawa.
Baada ya Manchester United kupoteza nafasi nyingi za wazi, Anthony Martial akaifungia bao la pili dakika ya 48, hiyo pia ikiwa ni kazi nzuri kutoka kwa Mkhitaryan.
Martial akafunga tena dakika ya 62 kabla ya Ibrahimovic kuhitimisha ushindi dakika ya 90 huku kiungo mkongwe  wa Ujerumani Bastian Schweinsteiger akicheza mchezo wake wa kwanza tangu mwezi Machi. Schweinsteiger aliingia dakika ya 86 kuchukua nafasi ya Martial. 
Anthony Martial scored two of Manchester United's four goals as they made it to the EFL Cup semi-finals

Anthony Martial akifunga moja ya mabao yake
Martial pictured putting the ball into the top left corner to score Manchester United's second goal after half time

Martial akiifungia Manchester United bao la pili
Zlatan Ibrahimovic and Martial were Manchester United's goalscorers on Wednesday night in the EFL Cup

Zlatan Ibrahimovic na Martial wote walifunga mabao mawili kila mmoja

Comments

comments

About Saluti 5

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *