MANCHESTER UNITED YAJIWEKA PAZURI KATIKA KUWANIA SAINI YA BEKI VICTOR LINDELOF WA BENFICA


Manchester United imepiga hatua kubwa katika kusaka saini ya beki wa Benfica Victor Lindelof mwenye thamni ya pauni milioni 38.

Ujumbe wa klabu hiyo ya Ureno ulikwenda England Jumatatu kwaajili ya mazungumzo zaidi na Manchester United chini ya mtendaji wake Ed Woodward ili kukamilisha dili la beki huyo mwenye umri wa miaka 22.

Kocha  Jose Mourinho amepania kuimarisha safu yake ya ulinzi katika dirisha la usajili la mwezi Januari akihofia kukosekana kwa sentahafu wake Eric Bailly ambaye atakuwa kwenye michezo ya Kombe la mataifa ya Afrika. 

No comments