MANCHESTER UNITED YASEMA BADO HAIJAMALIZANA NA VICTOR LINDELOF


MANCHESTER UNITED imesema bado haijapeleka ofa  juu ya usajili wa beki wa Benfica Victor Lindelof licha ya kuwepo mazungumzo baina ya klabu hizo mbili.

Wakala wa Victor Lindelof, Jorge Mendes amekuwa akizungumza kwa niaba ya Benfica, lakini United imesisitiza kuwa hakuna dili iliyofikiwa juu ya sentahafu huyo mwenye umri wa miaka 22.

Benfica inataka kulipwa pauni milioni 38 pamoja kuwepo kwa kipengele cha malipo ya ziada kadri beki huyo atakavyokuwa na mafanikio Old Trafford.

Jose Mourinho ana hofu ya kumpoteza  Eric Bailly kwaajili ya michuano ya  African Cup of Nations katika hatua hii ngumu ya msimu na anataka kuhakikisha kuwa anaongeza beki mpya.

No comments