MAOFISA WA MANCHESTER UNITED WAELEKEA KUCHOSHWA NA TABIA ZA JOSE MOURINHO

MAOFISA wa Manchester United wameanza kuchoshwa na tabia za kocha wao Jose Mourinho.

Mouroinho yuko hatarini kusimamishwa kukaa kwenye benchi la ufundi baada ya kutolewa uwanjani na mwamuzi Jon Moss dhidi ya West Ham.

Alitolewa kufuatia kitendo cha kupiga chupa teke kupinga nyota wake Paul Pogba kuonyeshwa kadi ya njano kwenye mechi ya West Ham.


Maofisa wa Manchester wanalalamika kichinichini kitendo cha kocha huyo kutuhumiwa makosa ya chama cha soka cha England (FA) kwa mara ya tatu katika kipindi cha mwezi mmoja.

No comments