Habari

MARCO VERRATTI AZIPONDA BARCELONA, REAL MADRID

on

KIUNGO wa timu ya Paris
Saint-Germain, Marco Verratti ni kama kaziponda timu za Barcelona na Real
Madrid baada ya kusema kuwa hazina ubavu wa kushinda mabao 5-0 kama zingekuwa
zinashiriki kwenye michuano ya igi Kuu Ufaransa “Ligue 1” kama zinavyofanya
kwenye La Liga.
Akizungumza juzi Verratti
ambaye amekuwa akikipiga kwenye klabu hiyo ya PSG tangu mwaka 2012 alisema kuwa
Ligi yao imekuwa haipewi umuhimu wa kutosha kama zilivyo nyingine kubwa Ulaya.
Muitaliano huyo alisema kwamba
ushindani na ubora uliopo katika Ligue 1 ni mkubwa na hivyo haoni kama Barca na
Madrid kama zingepamba kama zingekuwa zinacheza kwenye Ligi sawa.
“Nchini Ufaransa kuna ushindani
mkubwa hata kama timu inashika nafasi ya chini kwenye msimamo na timu hizo ni
ngumu unapokutana nazo,” Verrati aliandika kwenye ukurasa wa mtandao wa Goal.
“Katika ushindani mwingine mbio
zipo tofauti. Kwa mfano nchini Hispania kwa wastani timu kama hizo zinapokutana
na eal Madrid ama Barcelona huwa zinasahau ushindani na kucheza soka. Huwa
zinatoa mwanya badala ya kulinda,” aliongeza nyota huyo.

Alisema kuwa jambo hilo ndilo
linafanya Real Madrid ama Barcelona kufunga mabao matano ama zaidi na huku
akisisitiza kwamba hana uhakika kama zingeweza kufanya hivyo kama zingekuwa
zinacheza nchini Ufaransa.

Comments

comments

About Saluti 5

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *