MASHAUZI CLASSIC HAPATOSHI X-MAS MANGO GARDEN …nyimbo mpya kutambulishwa


UNAAMBIWA siku ya X-Mas Kinondoni yote burudani ya ukweli ni moja tu– Mashauzi Classic ndani ya Mango Garden.

Mashauzi Classic inayoongozwa na mwimbaji bora wa kike wa taarab Isha Mashauzi, itarindima ndani ya Mango Jumapili hii na kwa mara ya kwanza nyimbo mpya zitakazounda albam ijayo ya “Kismet” zitaanza kusikika.

Kwa wiki mbili sasa Mashauzi wamekuwa wakiendelea na mazoezi ya kupika nyimbo mpya ambapo Isha Mashauzi ameiambia Saluti5 kuwa siku ya X-Mas baadhi ya nyimbo mpya zitaanza kusikika ukumbini.

Leo Alhamisi Mashauzi hawatakuwepo Mango Garden ili kujifua zaidi na onyesho laa la X-Mas.

No comments