Mashauzi Classic Modern Taarab wamepania kufanya show kubwa zaidi leo usiku ndani ya Mango Garden, Kinondoni ili iwe zawadi mahsusi ya kuaga mwaka kwa mashabiki wao.

Mkurugenzi wa kundi hilo, Isha Mashauzi ameiambia Saluti5 kuwa onyesho la leo wanalichukulia kwa uzito wa hali ya juu na hivyo watahakikisha wanaachia burudani kubwa kuliko zote walizowahi kufanya ndani ya ukumbi wao huo wa nyumbani kwa mwaka huu.

“Tutakuwa na mchanganyiko wa muziki mzuri, nyimbo mpya na za zamani, taarab na vinjo vingine,” alisema Isha Mashauzi.
USISAHAU KUBONYEZA SUBSCRIBE HAPO
LIKE PAGE YETU YA FACEBOOK Saluti5

Post a Comment

 
Top
Nicolaus Trac