Habari

MASHAUZI CLASSIC KULA X-MAS MANGO GARDEN KINONDONI …bendi zingine ‘zote’ ziko Moro, Twanga Nyanda za juu Kusini

on

KUNDI la
Mashauzi Classic limeweka wazi ratiba yake ya sikukuu ya X-Mas.
Meneja wa
Mashauzi Classic Ismail Rashid “Sumaragar”, ameiambia Saluti5 kuwa X-Mas ambayo
itaangukia Jumapili ya tarehe 25 mwezi huu, kundi lao litakuwa Mango Garden
Kinondoni jijini Dar es Salaam.

“Bado tupo
kwenye mazungumzo na mapromota kuhusu show za mkesha wa X-Mas na Boxing Day,
lakini X-Mas yenyewe tutakuwa Mango Garden,” alisema Sumaragar.
Wakati Mashauzi Classic wakiwa Mango Garden X-Mas, karibu bendi zote zitakuwa Morogoro katika onyesho maalum litakalofanyika uwanja wa Jamhuri tarehe 25 Disemba.
Bendi hizo ni pamoja na Jahazi Modern Taarab, East African Melody, Sikinde, Msondo, Wakali Wao, Ogopa Kopa na FM Academia huku Twanga Pepeta wao wakiwa katika ziara ya mikoa ya Nyanda za Juu Kusini. 

Comments

comments

About Saluti 5

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *