MASHAUZI CLASSIC NDIYO BURUDANI KUBWA KULIKO ZOTE LEO USIKU X-MAS MANGO GARDEN


HATIMAYE siku imewadia! Kama wajanja wa mjini wanavyosema siku ya X-Mas Kinondoni yote burudani ya ukweli ni moja tu– Mashauzi Classic ndani ya Mango Garden.

Mashauzi Classic inayoongozwa na mwimbaji bora wa kike wa taarab Isha Mashauzi, itarindima ndani ya Mango leo usiku na kwa mara ya kwanza nyimbo mpya zitakazounda albam ijayo ya “Kismet” zitaanza kusikika.

Kwa wiki mbili sasa Mashauzi wamekuwa wakiendelea na mazoezi ya kupika nyimbo mpya ambapo Isha Mashauzi ameiambia Saluti5 kuwa siku ya X-Mas baadhi ya nyimbo mpya zitaanza kusikika ukumbini.

No comments