MASHUJAA BAND KUFUNGA MWAKA LINDI LEO USIKU … kesho wako Masasi


KUNDI lililokarabatiwa upya – Mashujaa Band, leo usiku litakuwa mjini Lindi katika onyesho kabambe la kufunga mwaka.

Mkurugenzi wa Mashujaa Band  Maxi Luhanga ameiambia Saluti5 kuwa onyesho hilo la mkesha wa mwaka mpya litafanyika Bwalo la Polisi ambapo wakazi wa Lindi watashuhudia utambulisho wa wasanii wapya na nyimbo mpya za Mashujaa.

Kama vile hiyo haitoshi, kesho Mwaka Mpya, Mashujaa Band watahamishia uhondo wao katika mji wa Masasi ndani ya ukumbi wa Iwawa Night Club.

Moja ya ngoma mpya ya Mashujaa Band ni “Thamani ya Mapenzi” ambayo inakimbiza kw asana kwenye vituo vya radio.

No comments