MAURCIO POCHETTINO AMVULIA KOFIA HARRY KANE... asema yupo katika kiwango kikubwa na ataisaidia timu msimu huu

MENEJA wa klabu ya Tottenham Hotspur, Maurcio Pochettino amemvulia kofia straika wake, Harry Kane kwa kusema yupo katika kiwango kikubwa na kwamba ataisaidia timu msimu huu.

Kisha akabainisha kuwa uwezo anaouonyesha ana matumaini makubwa kwa kikosi chake kupambana kwa ajili ya ubingwa wa premier msimu huu.

Akinukuliwa BBC, kocha huyo alisema mchezaji huyo ana sifa, nguvu na uwezo wa kuifaa sana klabu hiyo msimu huu.
“Amecheza vizuri katika kila mechi lakini uwezo binafsi wa kupambana kwa ajili ya timu ndio sifa inayomweka katika kiwango cha juu.”

“Amekuwa akipambana kwa ajili ya ushindi haya katika kipindi ambacho timu imekuwa nyuma ya matokeo dhidi ya timu pinzani, anahangaika katika kila idara kuhakikisha tunashinda,” alisisitiza meneja huyo.

Meneja huyo alikuwa anajibu maswali kuhusu umuhimu wa mchezaji huyo kwa klabu hiyo kwenye kikao na wanahabari katika kituo cha mafunzo ya klabu hiyo London.


Pochettino raia wa Argentina alijiunga na Spur Mei, 2014 kwa mkataba wa miaka mitano na Mei mwaka huu aliongeza mkataba huo na kuahidi kusalia White Hart Lane hadi 2021.

No comments