MAUWA TEGGO KUJA NA BONGE LA SURPRISE UTAMBULISHO WA YAH TMK LEO USIKU DAR LIVE


UTAMBULISHO wa bendi mpya ya taarab - Yah TMK Modern Taarab unafanyika leo usiku ndani ya ukumbi wa Dar Live jijini Dar es Salaam.

Bendi hiyo imeshaachia nyimbo nne kali “Sina Pupa”, “Kibaya Kina Mwenyewe”, “Figisu” na “Siwaguni wala Siwakohoi”, lakini kama vile hiyo haitoshi, leo usiku kutakuwa na zawadi bab kubwa kutoka kwa mmoja wa waimbaji bora kabisa wa kike kwenye taarab – Mauwa Teggo.

Mwimbaji huyo atatambulisha rasmi wimbo wake unaokwenda kwa jina la “Hashuo la Mke Mwenza Halininyimi Usingizi”.

Haya kazi kwenu mashabiki wa taraab …huyo ndo Mauwa Teggo “Makaa ya Mawe”.

No comments