Habari

MH. JOHN SHIBUDA SI KWA MANENO HAYA KUHUSU MASHAUZI CLASSIC!! …wapinzani wa Isha hebu someni hapa

on

MWANASIASA maarufu  mwenye
weledi wa hali ya juu wa kuzungumza Kiswahili fasaha, Mheshimiwa John Shibuda, Alhamisi usiku alikuwa mgeni rasmi katika onyesho la miaka mitano ya kundi la
Mashauzi Classic na kuwasisimua mashabiki  katika dakika zake tano tu
alizotumia kuongea jukwaani.
Shibuda aliyeitumikia nafasi ya ubunge jimbo la Maswa Magharibi tangu
mwaka 2005, akatumia muda huo mfupi kumpongeza Isha Mashauzi na bendi yake ya
Mashauzi Classic, hiyo ikiwa ni ndani ya ukumbi wa Mango Garden Kinondoni.
Mwanasiasa huyo alitiririka kama hivi: “Nichukue fursa hii kumpongeza
Isha kwa kuiongoza bendi yake bila kuterereka kwa miaka mitano.

“Isha ulipoanzisha bendi yako wengi walisema ni moto wa mabua lakini
leo nawaambia Mashauzi ni moto wa sola, HAUZIMIKI.
“Jamani ‘Aliyepewa na Mola Hapokonyeki’. Isha kapewa kipaji na Mola hivyo huwezi kukipora. Lakini pia waswahili wanasema ‘Gunia tupu halisimami’. Isha sio gunia tupu bali
ni gunia lilolojaa ndio maana linasimama.
“Niwaambie jambo moja, endeleeni kuwaombea maisha marefu wale wanafiki,
wazandiki na wasioitakia mema Mashauzi Classic, lakini sio maisha marefu na mazuri
kama ya peponi bali waishi wakiwa wamefumba macho kama wafu”.
Muda wote aliokuwa akiongea, Shibuda alikuwa akishangiliwa katika kila
nukta huku mashabiki wa Mashauzi wakitamani andelee kuongea na kumimina
sindano za moto kwa wale wasioitakia mema Mashauzi.
 Mheshimiwa Shibuda (katikati) akitema cheche
 Mheshimiwa Shibuda  akikata keki
  Mheshimiwa Shibuda  akimlisha keki Isha Mashauzi
  Mheshimiwa Shibuda  akilishwa keki na Isha
  Mheshimiwa Shibuda  akiwa na Isha
 Mheshimiwa Shibuda  jukwaani. Kulia ni meneja wa Mashauzi Classic Sumaragar

Comments

comments

About Saluti 5

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *