MISULI YA NYAMA ZA PAJA KUMWEKA BONUCCI NJE YA DIMBA MIEZI MIWILI

KLABU ya Juventus imetangaza kuwa nyota wao Leonardo Bonucci alilazimika kukaa nje ya uwanja kwa muda wa miezi miwili kutokana na majeraha ya misuli ya nyama za paja yanayomkabili.

Taarifa hiyo imekuja baada ya nyota huyo wa timu ya taifa ya Italia Jumapili kulazimika kutolewa nje ya uwanja wakati wa mchezo ambao mabingwa hao wa Ligi Kuu ya serea A wakifungwa na Genoa 3-1, kwenda kufanyiwa vipimo baada ya kikosi hicho kurejea mjini Turin.

Na kwa sasa jeraha hilo ambalo alilipata kwenye paja lake la kushoto litamfanya Bonucci akae nje ya uwanja walau hadi katikati ya Januari.


“Jeraha la misuli ya nyama za paja kwenye mguu wake wa kushoto limebainika na litafanya aweze kupona kati ya siku 45 hadi 60 ,” ilieleza taarifa hiyo ya Juve iliyotolewa juzi.

No comments