MOURINHO ASEMA MAN UNITED HAWATAUZA MCHEZAJI BILA RIDHAA YAKE


KOCHA wa Manchester United Jose Mourinho ameendelea kusisitiza kuwa ana furaha na kikosi chake alichonacho.

Mourinho amesema hategemei kufanya mabadiliko makubwa kwenye dirisha dogo la Januari na kama ikibidi kusajili basi labda ni mchezaji mmoja tu.

Akizungumzia kikosi chake, Mourinho alisema ana kikosi kizuri na kwamba hana mpango wa kuuza mchezaji labda mchezaji atake mwenyewe.

“Kama tukimuuza mchezaji basi si kwasababu hatumuhitaji, ni kwasababu yeye ametaka kuondoka”, alisema Mourinho katika maongezi yake na Sky.

No comments