MOURINHO ASEMA NI PASUA KICHWA KUWA NA WACHEZAJI WENGI KWENYE NAFASI MOJA ...ajisikia vibaya kuwasotesha benchi Depay na Ashley Young


KOCHA wa Manchester United Jose Mourinho amesema anahisi hajatenda haki kwa Memphis Depay na Ashley Young kwa kushindwa kuwapa mechi za kutosha ili kuthibitisha ubora wao kwake.

Depay amecheza mara kumi chini ya Mourinho na amekuwa akihusishwa kwa karibu na uhamisho wa kwenda Everton mwezi Januari. Ashley Young yeye amecheza mechi tisa chini ya Mourinho.

"Najisikia vibaya kwa sababu sikutoa nafasi kubwa kwa kila mmoja," Mourinho aliiambia Sky.

"Katika nafasi ya ushambuliaji wa pembeni hatuna mawinga asilia lakini tuna watu wengi ambao wanaweza kucheza pale. Katika eneo hilo tumewaongeza Rashford na Rooney ambao wanaungana na wachezaji kama Lingard, Mata, Mkhitaryan, Memphis Depay, Martial na Ashley Young. 

"Wakati mwingine kuwa na wachezaji wengi kwenye nafasi moja inaumiza kichwa. Nakiri kuwa sikuwapa nafasi ya kutosha Depay na Young, jambo linalofanya nijisikie vibaya kwa kiasi fulani."
No comments