MOURINHO, RONALDO WADAI KUSILIBIWA TUHUMA ZA KUKWEPA KULIPA KODI

WAKALA wa Cristiano Ronaldo na Jose Mourinho amewatetea wateja wake akidai kuwa tuhuma wanazopewa za kukwepa kodi zina lengo la kuwachafulia.

Jorge Mendes ametoa kauli hiyo baada ya madai kuwa wawili hao wana tuhuma za kukwepa kodi nchini Hispania.

Magazeti yapatayo 12 kwa umoja wao, yamedai ndani ya wiki tatu zijazo yatachapisha taarifa za namna wanamichezo hao wanavyoingia mitini kulipa kodi barani Ulaya.

Mvujo wa tarifa hizo unadai kuwa nyota wa Real Madrid, Ronaldo na kocha wa Manchester United, Mourinho ni miongoni mwa wanamichezo wanaotuhumiwa kukwepa kodi.


Ronaldo anadaiwa kukwepa kulipa kiasi cha euro mil 150 tangu mwaka 2009 alipojiunga na Real Madrid akitumia akaunti za benki zilizoko kwenye visiwa vya Virgin vilivyoko Uingereza.

No comments