MPENZI WA ZAMANI WA SHILOLE ATEMA CHECHE

MPENZI wa zamani wa Shilole, Hamadai amefunguka na kueleza jinsi alivyokutana na Shilole na kuanza mahusiano.

Mwimbaji huyo mchanga wa Bongofleva alifahamika mara baada ya kuwa na mahusiano na Shilole.

Mwimbaji huyop amesema kuwa kwa sasa ameamua kuachana kabisa na Shilole kwa sababu kuna mambo ambayo alikuwa akiona hayaendi sawa kabisa na sasa ameamua kujikita katika kuziki wake.

“Shilole ndie aliyenitongoza mimi na sikumuanza, sasa nimeona niachane nae kwa sababu kuna vitu ambavyo nilikuwa naviona haviendi sawa. Pia mimi siwezi mzungumzia vibaya kwani kabla yangu alikuwa na watu kadhaa ambao tayari ameachana nao,” alisema msanii huyo.


“Akawa na mimi na tukaachana na sasa ana mtu mwingine ambaye pia anaweza kuachana naye, hayo ni maisha yake na mimi siwezi kumwingilia,” aliongeza Hamadai.

No comments