MSONDO NA SIKINDE KUTIFUANA TCC CLUB MKESHA WA MWAKA MPYA


Msondo Ngoma Music Band na Mlimani Park Orchestra “Sikinde Ngoma ya Ukae” zitaumana vikali kwenye viwanja vya CDS Park (zamani TCC Club) Chang’ombe jijini Dar es Salaam siku ya mkesha wa Mwaka Mwaka.

Onyesho hilo litapigwa tarehe 31 mwezi huu, wiki moja tu baada ya bendi hizo kukutana jukwaa moja mjini Morogoro siku ya X- Mas.


Kama ilivyo ada, tayari mashabiki wa bendi hizo mbili kongwe, wameanza kutambiana juu ya mtanange huo wa mkesha wa Mwaka Mpya.

No comments