MWANA FA ATAKA VYOMBO VYA HABARI WALIPOTEZEE BIFU LA DIMPOZ, DIAMOND

MWANA FA amesema kuwa njia pekee ya kuzima  bifu la Dimpoz na Diamond ni kuacha kulizungumzia mara kwa mara kwenye vyombo vya habari ili watu walisahau.

“Umefika wakati sasa kila mmoja wetu anyamaze kwani kuendelea kuzungumzia bifu hilo ni sawa na kukuza ugomvi ambao kimsingi haupaswi kuwepo,” alisema FA.

Alisema kuwa hakuna haja ya kufanya upambe kama ilivyo sasa kwa madai kwamba hali hiyo huenda wabaya wao wakajiingiza kati na kuwafanyizia na hivyo kusababisha hatari.


“Mimi niliulizwa nikaeleza kile ninachokiona kwamba tujiwekee mipaka kama binadamu, watu wanyenyekee warudi chini kidogo, lakini kikubwa zaidi ni kwamba suala la wasanii wetu lisiendelee kuzungumzwa ama kutangazwa," alisema.

No comments