MWANAFA ASEMA HANA HAJA YA KUTOA ALBAMU KWA SASA

MWANA FA amesema hajatoa albamu kwa zaidi ya miaka mitano sasa kutokana na kile alichodai kuwa ni kukosekana kwa kile alichokiita “uwekezaji wa kueleweka” katika muziki nchini.

Alisema kuwa tangu alipofyatua albamu ya “Habari Ndio Hiyo” hajatoa nyingine na ataendelea kusubiri kwanza hadi hapo atakapojirihisha kuwa akiitoa hatopata hasara.

“albamu yangu ya mwisho ni ile ya “Habari Ndo Hiyo”, ambayo niliitoa zaidi ya miaka mitano iliyopita na bahati mbaya haikufanya vizuri sokoni ingawa ilikuwa na nyimbo zilizoshiba,” alisema MwanaFA.

Rapa huyo ambaye hivi sasa anatamba na wimbo wake wa “Dume Suruali” alisema kuwa hawezi kutoa albamu kwa sababu tu mashabiki wanataka bali anaangalia kama inaweza kusambazwa kila kona ya nchi na akapata mafanikio.       

No comments