MWANAMKE WA NAY WA MITEGO AGOMA KUUZISHWA SURA

MWANAMKE ambaye amemfanya rapa Nay wa Mitego aandike wimbo “Sijiwezi” hataki habari za kuuzishwa sura katika mitandao ya kijamii kaa ilivyo kwa wapenzi wengine wa rapa huyo waliopita.

Akizungumza wiki hii, Ney alisema hawezi kufanya kitu ambacho hapendi mwanamke huyo na ataendelea kuheshimu maamuzi yake huku akikiri kuwa ni jambo gumu kwake kwakuwa alishazoea ku-share picha za wapenzi wake kwenye mitandao ya kijamii.

“Huyu niliyenae kwa sasa hataki kusikia kuhusu masuala ya kuweka sijui picha kwenye mitandao,” alisema Nay.


“Ni mwanamke fulani ambaye ana msimamo wake kuhusu maisha yake, hataki masuala ya kuyumbishana katika mapenzi,” alisema.

No comments