MKURUGENZI wa michezo wa timu ya PSG Patrick Kluivert amesema kuwa japo wana hamu ya kumsajili straika Neymar lakini hawatatumia mwanya wa kesi inayomkabili stasa huyo.

Kwa muda mrefu mabingwa hao wa michuano ya Ligue 1 wamekuwa wakihusishwa kutaka kumsajili nyota huyo mwenye umri wa miaka 24 na ambaye anasemekana kuwa miongoni mwa wachezaji wenye vipaji.

Neymar alisaini mkataba mpya na Barca Oktoba mwaka huu lakini uhamisho wake wa mwakac 2013 kutoka katika timu ya Santois kwenda Nou Camp umeendelea kutiliwa shaka nchini Hispania.


Jumatano wiki iliyopita mwendesha mastaka Jose Perais aliomba nyota huyo na baba yake wahukumiwe kifungo cha miaka miwili pamoja na faini ya euro mil 10 na pia mama yake afungwe mwaka mmoja kutokana na mazingira ya rushwa yaliyopo katika uhamisho.
NENDA PLAY STORE KUPITIA SMART PHONE YAKO KISHA DOWNLOAD APP YETU YA "SALUTI5">>>> BONYEZA HAPA
LIKE PAGE YETU YA FACEBOOK Saluti5

Post a Comment

 
Top
Nicolaus Trac