NI UHONDO JUU YA UHONDO MIAKA MITANO YA MASHAUZI CLASSIC LEO USIKU MANGO GARDEN


LEO usiku ndiyo linafanyika lile onyesho kabambe la kusherehekea miaka mitano ya Mashauzi Classic ndani ya Mango Garden Kinondoni.

Kundi la East African Melody litakuwepo Mango Garden kusindikiza onyesho hilo la Mashauzi Classic.

Mkurugenzi wa Mashauzi Classic, Isha Mashauzi ameiambia Saluti5 kuwa kutakuwa na mambo mengi ya kuvutia, zikiwemo burudani kibao kutoka kwa wasanii nyota wa taarab wa bendi mbali mbali.

“Hili ni onyesho letu maalum, miaka mitano bila kulegalega ni jambo la kumshukuru Mungu, kwahiyo tunataka kuwapa mashabiki wetu vitu adimu,” alisema Isha.

“Tunashukuru kuwa tunao wasanii ndugu zetu ambao wameahidi kuja kutupa  sapoti kitu ambacho kwa namna moja au nyingine kitasaidia kulinogesha onyesho la leo,” aliongeza Isha Mashauzi.

Onyesho hili pia litakuwa linaifanya Mashauzi Classic itimize miaka mitano ndani ya ukumbi wa Mango Garden. 

No comments