"NILIJIUNGA SEVILLA KWA KUVUTIWA NA MSOSI NA MADEMU WA KIHISPANIA" SAMIR NASRI AFUNGUKA

STAA Samir Nasri alijiunga na Sevilla ya Hispania baada ya kuvutiwa na chakula na wasichana wazuri wa Kihispania.
Nasri alijiunga na Sevilla  msimu huu akitokea Manchester City.

Nasri amefunga mabao matatu katika mechi 13 alizoichezea Sevilla msimu huu.

Alisema kuwa aliamua kuondoka Manchester City licha ya kutakiwa kubaki na kocha Pep Guardiola.


“Niliwauliza nyota wa Hispania David Silva, Jesus Navas na Norito juu ya maisha ya Hispania wakaniambia kuna chakula kizuri na wasichana warembo na Guardiola alimfagilia kocha wa Sevilla, Juanma Lillo. Nikaona ni vitu sahihi kwanza.”

No comments