NISHA AGOMA KUMTAJA "BABA KIJACHO" WAKE... Barakah Da Prince, Nay wa Mitego,Minu Calypto wahusishwa

SALMA Jabu “Nisha” amesema kuwa piga ua hatamtaja mtu aliyempachika ujauzito kama ambavyo amekuwa akiombwa kufanya, kwa madai kwamba haoni sababu ya kufanya hivyo.

“Watu wamekuwa wananiuliza sana kuhusu mimba, hasa bada ya mimi mwenyewe kuweka wazi kwenye mitandao ya kijamii, lakini sijawahi kumtaja kwa jina mhusika wa mimba na siwezi kufanya hivyo,” amesema Nisha.

Amesea kuwa anachojua ni kwamba aliyempa mimba walishaachana na aligundua wakati tayari yuko hivyo na ameahidi kumlea mtoto huyo mwenyewe bila sapoti ya “baba kijacho” huyo kwa vile uwezo anao.


Nyota wa Bongofleva, Barakah Da Prince, Nay wa Mitego na msanii wa Kizazi Kipya anayeinukia, Minu Calypto wamehusishwa na ujauzito huo katika mitandao ya kijamii na wote wamekana kuutambua. 

No comments