ONYESHO LA MSONDO NA SIKINDE LAOTA MBAWA …sasa kupigwa Januari 14 Leaders Club


Kisicho riziki hakili, ndivyo unavyoweza kusema baada ya mpango wa kuwakutanisha mahasimu wa dansi -Msondo na Sikinde kushindikana mara mbili mfulilizo.

Msondo na Sikinde ilikuwa ziumaune leo usiku kwenye viwanja vya TCC Club, lakini onyesho limeahirishwa kufuatia ukumbi huo kukosa kibali cha kufanya shughuli za burudani.

Siku ya X-Mas Msondo na Sikinde walitarajiwa kukutana jukwaa moja mjini Morogoro lakini bendi zote mbili hazikuibuka mjini humo baada ya promota kukiuka makubaliano.

Saluti5 imetaarifiwa kuwa onyesho la Msondo na Sikinde sasa litafanyika Leaders Club siku ya Jumamosi ya Januari 14 na huenda wakasindikizwa na Twanga Pepeta.

No comments