OZIL AWAJIBU WANAOMPONDA... aweka rekodi ya kutoa pasi nyingi za mabao Ligi Kuu England

MESUT Ozil amewajibu wanaomponda kwa kuweka rekodi ya kutoa pasi nyingi za mabao kwenye Ligi Kuu England.

Ozil alipiga krosi iliyounganishwa na Olivier Giroud ambaye alifungia bao Arsenal kwenye dakika za mwisho kwenye mechi dhidi ya West Bromwich Arbion juzi.

Mjerumani huyo ambaye aliichezea Arsenal kwa mara ya 100 akifikisha pasi 36 za mabao, anakuwa mchezaji wa pili nyuma ya nyota wa zamani wa Manchester United, eric cantona kwa kutoa pasi nyingi za mabao katika mechi 100.

Cantona alikuwa ametoa pasi 39 za mabao alipofikisha mechi 100.

No comments