Habari

PICHA 10: ISHA MASHAUZI ALIVYOTESA KATIKA UZINDUZI WA KAMPENI YA KUTOKOMEZA UKATILI DHIDI YA WANAWAKE NA WATOTO

on

JUMANNE ya wiki hii, mwimbaji bora wa kike wa
taarab, Isha Mashauzi, alikuwa msanii pekee aliyeburudisha katika uzinduzi wa Mpango
kazi wa Taifa wa Kutokomeza Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto 2017/ 18-2021.
Uzinduzi huo uliofanyika katika ukumbi wa Julius
Nyerere International Convention Centre (JNICC) jijini Dar es Salaam, uliongozwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy
Mwalimu na kushuhudiwa na viongozi wengi wa serikali wakiwemo mawaziri kadhaa.
Isha Mashauzi akatandika ‘live’ burudani ya
nguvu kupitia vibao vyake vya taarab pamoja na wimbo maalum alioutunga kwaajili
ya kampeni hiyo.


Hizi ndio ‘chanel’ zinazopaswa kutafutwa na wasanii na sio akili zao kubakia kwenye show za ukumbini peke yake. Keep it Up.
Zifuatazo ni picha 10 za Isha Mashauzi  na kundi lake ndani ya ukumbi wa Julius
Nyerere International Convention Centre.
 Isha Mashauzi akishusha burudani ya nguvu
 Isha akiendeleza makamuzi
 Isha akiandika dondoo muhimu
 Isha akiwakoroga hadi wazungu
 Wazungu wanamtunza mshiko
 Hakika muziki haunaga rangi
 Isha akiendelea kufanya vitu vyake
Mandhari ya ukumbi wa Julius Nyerere International
Convention Centre.

Waziri wa Afya , Maendeleo ya Jamii, Jinsia,
Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu (kushoto) katika picha ya pamoja na Isha 

Waziri wa Afya , Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu (kulia) katika picha ya pamoja na Saida Ramadhani

Comments

comments

About Saluti 5

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *