PICHA 11: MASHAUZI CLASSIC ILIVYOMIMINA UHONDO WA X-MAS MANGO GARDEN …wimbo mpya wa Isha Mashauzi ni noma!!!KUNDI la Mashauzi Classic usiku wa kuamkia leo, lilimimina uhondo si wa kitoto kwenye ukumbi wa Mango Garden Kinodoni katika maadhimisho ya sikukuu ya X-Mas.

Mashabiki waliofurika Mango Garden wakashuhudia kundi hilo likitesa na ‘playlist’ tamu iliyowafanya wasikae kwenye viti vya na kujimwaga katika ‘dancing floor’ kucheza kugoma la Mashauzi.

Kama ilivyotangazwa hapo awali kuwa kundi hilo litatambulisha nyimbo zao mpya kabisa, ndivyo ilivyokuwa ambapo waimbaji chipukizi Mariam na Rahma Aman wakaibuka na vigongo vipya kabisa.

Mariam akatambulisha wimbo unakwenda kwa jina la “Huyu ni Wangu” na Rahma akatesa na kitu “Kisicho Riziki Hakiliki”.

Nyimbo hizo zitakuwepo kwenye albam ijayo ya “Kismet” ambayo itakuwa na jumla ya nyimbo sita.

Lakini kama kuna jambo lililoteka show, basi ni wimbo mpya kabisa wa Isha Mashauzi “Radhi ya Mama Haina Mbadala” ambao licha ya kuwa ulikuwa unasikika kwa mara ya kwanza, ukauzibua ukumbi wa Mango kwa shangwe kutokana na ujumbe na melody alizokuwa akizitumia Isha.

Kwenye ngoma chini ya wimbo huo nako pia kulikuwa na balaa, Isha alijaza vionjo vilivyoteka masikio ya mashabiki, mpangilio wa upigaji vyombo ukawafaya watu waucheze kwa shauku na masham sham ya hali ya juu.

Isha akaimbia Saluti5 kuwa wimbo huo pia utapatikana katika albam ya “Kismet”.

Pata picha 11 za onyesho hilo la Mashauzi Classic ndani ya Mango Garden.
 Asia Mzinga jukwaani
 Hashim Said akiimba wimbo "Bonge la Bwana"
 Isha Mashauzi akimimina uhondo
 Isha Mashauzi na daftari lake la wimbo mpya kabisa
 Kali Kitimoto akipapasa kinanda
 Isha akitambulisha wimbo wake mpya kabisa

Mashabiki wakicheza wimbo mpya wa Isha Mashauzi
 Mkude kwenye solo gitaa
 Saida Mashauzi jukwaani
 Saida Mashauzi akipagawisha mashabiki wa Mashauzi
Shaabab wa Kumwaga kwenye bass

No comments