PICHA 14: ALLY J, MOSI WANG’ARA ONYESHO LA JAHAZI MANZESE


WASANII wapya wa Jahazi Modern Taarab Ally J mkali wa kinanda pamoja na mwimbaji Mosi Suleiman, walikuwa kivutio cha onyesho la bendi hiyo Jumapili usiku katika ukumbi wa Lunch Time Manzese.

Ally Jay alitesa katika nyimbo kadhaa ukiwemo “VIP” huku Mosi akichanua vilivyo kupitia wimbo “Maneno ya Mkosaji” wa Leyla Rashid na “Mkuki kwa Nguruwe” wa Hadija Yussuf.

Mosi aliimba kwa ufasaha nyimbo hizo huku akichomekea vionjo fulani kwenye ngoma vilivyowatia wazimu mashabiki wa Jahazi.

Nyota wengine waliong’ara kwenye onyesho hilo ni pamoja na waimbaji Prince Amigo, Mishi Zere, Fatma Kassim, Mwasiti Kitoronto na Zubeida Mlamali huku Jumanne Ulaya akifunika kwa sana kwenye gitaa la solo.

Yote kwa yote onyesho hilo lilidhihirisha kuwa Jahazi bado iko imara sana.
 Ally Jay akipapasa kinanda
  Ally Jay akikusanya kijiji jukwaani
 Fatma Kassim
 J Four Boya wa Mashauzi akisalimia jukwaa la Jahazi
 Mariam Kasola wa Mashauzi Classic naye alikaribishwa jukwaani na kuimba wimbo "Sitaki Shari" wa Leyla Rashid
 Hawa ni mashabiki waliokuwa wakimshangilia Mosi Suleiman
 Mishi Zere ...huwa haaribu huyu mtu
 Mishi Zere akiimba kwa hisia kali
 Mosi na Amigo kwa raha zao jukwaani
 Mosi Suleiman alitia fora
 Pince Amigo "Mzee wa madongo" akiimba waimbo Tiba ya Mapenzi
 Waimbaji wa Jahazi jukwaani
 Watangazaji wa EFM wakitoa pongezi zaoo kwa Jahazi
Zubeida Mlamali bonge la kiraka katika Jahazi

No comments