Habari

PICHA 14: CHOKORAA NA KALALA JR WASHUHUDIA UTAMBULISHO WA BENDI MPYA YA FERGUSON NA ROGART HEGGA …inaitwa DSS Band “Wazee wa Kujilipua” …yumo pia Adolph Mbinga

on

MADAKTARI waajiriwa waanzisha zahanati yao, ndivyo wanavyofananisha
Rogart Hegga na Ferguson baada ya kutambulisha bendi yao mpya Jumamosi usiku.
Naam, Rogart Hegga na Ferguson wameanzisha bendi yao inayokwenda kwa
jina la DSS Band (Dar es Salaam Super Sound) “Wazee wa Kujilipua” na
wameitambulisha rasmi usiku wa kuamkia leo pale Family Bar, Tabata Mbuyuni
jijini Dar es Salaam. Kamera ya Saluti5 ilikuwepo.
Wasanii hawa wa Twanga Pepeta hawako peke yao katika mpango huu, bali
pia wapo madansa wawili wa kiume wa Twanga Mapande (Dogo White) na Maga, yumo
mpiga solo wa zamani wa Twanga Adolph Mbinga lakini pia kuna mwimbaji wa zamani
wa The African Stars Band kabla haijawa Twanga Pepeta, Kasuku Mbwana.
Mwimbaji wa TOT Band Atanas Montanabe naye pia ni miongoni mwa wasanii
wanaounda DSS Band.
Miongoni mwa watu maarufu walioshuhudia utambulisho wa DSS Band ni
pamoja na waimbaji wawili wa Twanga Pepeta Khalid Chokoraa na Kalala Jr.
Wasanii wote hao wa Twanga Pepeta (Rogart, Ferguson, Kalala Jr,
Chokoraa, Mapande na Maga) hawajasafiri na bendi yao mkoani Ruvuma kwa sababu
mbali mbali – kiafya, kikazi na kifamilia.
DSS Band ikapiga bonge la show iliyokwenda hadi saa 9 za usiku ambapo
nyimbo maarufu za wasanii hao kama vile “Fadhila kwa Wazazi”, “Neema”  na nyinginezo zilirindima huku pia wakitambulisha
wimbo mmoja mpya utunzi wake Rogart Hegga Katapila.
Je wasanii hawa wameondoka Twanga Pepeta? Hapana bado wako Twanga
Pepeta kama anavyosema Rogart Hegga:
“Sisi bado ni wasanii wa Twanga Pepeta, DSS Band inaundwa na wasanii
kutoka bendi tofauti na hakuna hata mmoja aliyeasi ofisi yake,” anaeleza
Rogart.
“Huu ni mradi wetu wa pembeni ili kujiongezea kipato, tutakuwa
tunafanya kazi siku ambazo bendi zetu hazina kazi na kama itatokea mwingiliano
basi tutaomba ruhusa mapema.
“Hii ni kama madaktari waajiriwa wanavyoamua kufungua zahati zao huku
wakiendelea kuwa watumishi watiifu kwenye hospitali zilizowaajiri,” alisema
Rogart Hegga katika maongezi yake na Saluti5 ukumbini hapo.
Aidha, Ferguson pia aliiambia Saluti5 kuwa mashabiki wao wa Twanga Pepeta
wasihofu kwani mradi huu haumaanishi kuwa wanahama bendi.
 Atanas Montanabe mwimbaji wa DSS Band
 Mpiga drum wa DSS Band
 Ferguson na Adolph Mbinga
 Ferguson akionyesha ishara ya kimyaaaa!
 Ferguson na Rogart (waliosimama) katika picha ya pamoja na Khalid Chokoraa, Catty Chuma na Kalala Jr wakati wa utambulisho wa bendi mpya ya DSS
 Kasuku Mbwana mmoja wa waimbaji wanaounda DSS Band
 Rogart Hegga
 Madansa Mapande (kushoto) na Maga
 Adolph Mbinga kwenye sola la DSS Band
 Juma Jerry wa TOT akisalimia kisanii jukwaa la DSS Band
 Rogart Hegga akiwajibika na DSS Band mkesha wa X-Mas
 Rose mwimbaji pekee wa kike wa DSS Bad
Side James kwenye bass gitaa

Comments

comments

About Saluti 5

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *