PICHA 32: MOTO WA YAH TMK SI WA KITOTO …UTAMBULISHO WAO WAITIKISA DAR LIVE …Teggo, Mcharuko, Vuvuzela tishio


ONYESHO la utambulisho wa bendi mpya ya taarab – Yah TMK Modern Taarab, lililofanyika jana usiku, lilitia fora.

Yah TMK ilizinduliwa ndani ya ukumbi wa Dar Live, Mbagala jijini Dar es Salaam na kusindikizwa na burudani kibao ikiwemo Twanga Pepeta, Malkia Leyla Rashid, Madada Sita, Dullah Makabila, Chegge na Temba sambamba na ‘sapraiz’ kutoka kwa Yamoto Band.

Kundi hilo jipya lililopanda jukwaani usiku wa saa 8 kasorobo, likamimina uhondo wa nyimbo saba mfululilizo ambazo ziliutikisa vilivyo ukumbi wa Dar Live.

Waimbaji wote wa Yah TMK walifanya vizuri sana, lakini hakuna ubishi kuwa Aisha Vuvuzela, Fatma Mcharuko na Omar Teggo ndiyo walioiteka show.

Wapiga vyombo wa Yah TMK Mohamed Mauji (solo) Mussa Mipango (bass), Chid Boy (kinanda) na Babu Ally Kichupa (kinanda) nao walitia fora kwa namna walivyoujaza muziki wa bendi yao.


Pata picha 32 za onyesho hilo la Yah TMK Modern Taarab.
Chaz Baba akishiriki na Twanga Pepeta kusindikiza uzinduzi wa TMK Modern Taarab
Chaz Baba (kushoto) na Ally Chocky wakilingurumisha goma la Twanga Pepeta
Ally Chocky wa Twanga
Ferguson wa Twanga Pepeta
Kushoto ni Juma Jerry wa TOT akifuatilia utambulisho wa Yah TMK Modern Taarab
Wadau wa muziki Juma Mbizo (kushoto) na Said Mdoe
Godi Kanuti wa Twanga Pepeta
Madada Sita nao wakiisindikiza Yah TMK
Malkia Leyla Rashid wa Jahazi naye alialikwa kuisindikiza Yah TMK
Malkia Leyla Rashid jukwaani
Martin Kibosho akipiga 'ndondo' kwenye jukwaa la Twanga Pepeta

Rogart Hegga wa Twanga Pepeta

Twanga Pepeta jukwaani
Boss wa Yah TMK Modern Taarab, akizungumza machache kabla bendi yake haijatambulishwa rasmi
MC alikuwa ni Mwasiti Robert, msanii wa zamani wa Jahazi Modern Taarab
Bi Mwanahawa Ally akiimba "Sina Pupa" moja ya nyimbo za Yah TMK
Bi Mwanahawa Ally 
Chidy Boy kwenye kinanda
Babu Ally Kichupa akipapasa kinanda
Waimbaji chipukizi wa Yah TMK wakitesa na moja ya nyimbo za bendi hiyo
Mandhari ya Dar Live jana usiku
Mohamed Mauji kwenye solo
Mauwa Teggo akiimba "Ashuo la Mke mwenza"
Fatma Mcharuko jukwaani
Fatma Mcharuko na wimbo "Siwaguni wala Siwakohoi"
Mussa Mipango kwenye gitaa la bass
Ilikuwa ni full shangwe
Omar Teggo jukwaani
Teggo akikwambia "Figisu Figisu Zimekwisha"
Aisha Vuvuzela
Vuvuzela na kitu "Kibaya Kina wenyewe"
Safu ya waimbaji wa Yah TMK Modern Taarab


No comments