Habari

PICHA 45: MIAKA MITANO YA MASHAUZI CLASSIC NI ZAIDI YA ‘SUPER’ …Mango Garden yazizima kwa uhondo wa burudani

on

WALISEMA haijai sasa inamwagika! Ndivyo unavyoweza kusema juu la
onyesho la miaka mitano ya Mashauzi Classic lililofanyika Alhamisi usiku na
kufana sana.
Onyesho hilo lililofanyika Mango Garden Kinondoni, lilihudhuriwa na
umati mkubwa wa watu na kusababisha mashamsham ya kila aina kutoka kila kona ya ukumbi.
Ilikuwa kama movie flani hivi ambapo saa 3 usiku ukumbi ulikuwa mweupe
bila shabiki yeyote. Saa 4 usiku wakaanza kuonekana mashabiki wa kuhesabika.
Saa 5 usiku heshima ikaanza kuonekana kwa watu kuingia kwa kasi kubwa ukumbini.
Saa 6 usiku na kuendelea ikawa ni nyomi si la kitoto.
The East African Melody ndiyo waliofungua pazia la burudani saa 4 za
usiku hadi 5.30, wakafuatia Mashauzi Classic na nyimbo zao tatu “Sijamuona kati
yenu” ulioimbwa na Rahma Aman, “Mapenzi Yamenivuruga” ukiimbwa na Mariam Kasola,
huku Asia Mzinga akishuka na “Ubaya Haulipizwi”.
Baada ya hapo MC wa onyesho hilo Prince Amigo  akaleta ‘surprise’ ya Jahazi Modern Taarab
ambao waliimba nyimbo mbili “Nia Safi Hairogwi” wa Mishi Zere na “Tiba ya
Mapenzi” kutoka kwa Amigo mwenyewe.
Mambo yakazidi kunoga,  akapanda jukwaani mkurugenzi wa Mashauzi Classic Isha
Mashauzi na kuimba wimbo wa “Nani Kama Mama” ambao uliibua shangwe nyingi.
Likafuata tendo la kupata risala fupi na tamu kutoka kwa Isha Mashauzi
juu ya historia fupi ya Mashauzi Classic, kisha zikafunguliwa shampeni tano
kabla keki haijakatwa na mgeni rasmi – mwanasiasa mkongwe John Shibuda ambaye pia
alizungumza machache ya kumpongeza Isha na bendi yake.
Unajua kilichofuata baada ya hapo? Ilikuwa ni ‘surprise’ nyingine, safari hii ikiwa ni kupandishwa jukwaani kwa mwimbaji wa zamani wa Mashauzi
Classic Ashura Machupa akaimba wimbo wake ambao hakubahatika kuurekodi “La
Mungu Halina Mwamuzi” na kushangiliwa sana na mashabiki waliofurika Mango
Garden. Lilikuwa jambo la kuvutia sana.
Isha akarejea jukwaani na wimbo “Nimpe Nani”, halafu akaja Abdumalick
Shaaban na “Kupendwa Bahati Yangu” kisha Saida Mashauzi na kitu “Pendo la
Ukakasi” kabla Isha hajafunga pazia la burudani na wimbo “Sura Surambi”.
Ilikuwa ni ratiba tamu isiyochusha, ratiba iliyokwenda shule, ratiba
iliyofanya kila mshabiki aone pesa yake imekwenda kihalali, labda tu kwa wale
mashabiki ‘virusi’ waliokwenda ukumbini kwa kazi maalum ya kusaka mapungufu.

Pata picha 45 za onyesho hilo la miaka mitano ya Mashauzi Classic ambazo zimewekwa kwa kufuata mtiririko mzima wa show hiyo.
MC wa onyesho alikuwa ni Prince Amigo kutoka Jahazi Modern Taarab
waimbaji wa Melody
Ramla wa Melody
 Hassan Sudi mpiga kinanda wa Melody
 Bi Mwanaidi Shaaban wa Melody
Rahma Aman wa Mashauzi Classic
Mariam Kasola “Mum Junior” wa Mashauzi
Asia Mzinga wa Mashauzi Classic
 Mishi Zere wa Jahazi akishambulia jukwaa
Mishi Mohamed “Mishi Zere”
 Jumanne Ulaya wa Jahazi
 Amigo wa Jahazi akisepa na kijiji
Ally Jay akipiga kinanda cha Jahazi kwa mara ya kwanza tangu arejee kundini
Mtu na meneja wake kwenye red carpet … ni Isha na Sumaragar
 Isha Mashauzi jukwaani
 Isha akiimba kwa hisia kali
Nyomi
Shabiki anayejulikana kwa jina la Fataki akiwa kwenye kilele cha furaha
Isha Mashauzi akisoma risala fupi
Shampeni tano
 Watu ambao ukiwakata damu yao inatoka na maandishi ya Mashauzi Classic …Mamuu Original (kushoto) na Judith Marcus
Isha baada ya kufungua shampeni yake
 Shangwe
Ally Jay na Isha
 Mh. Shibuda (katikati) akiongea machache
  Mh. Jonh Shibuda akiendelea kutiririka
Moja ya keki za miaka mitano ya Mashauzi Classic
  Mh. Shibuda akikata keki
  Mh. Shibuda akimlisha keki Isha
 Mh. Shibuda akilishwa keki na Isha
 Isha baada ya kumkaribisha jukwaani Ashura Machupa
 Ashura Machupa
Ashura Machupa akiimba “La Mungu Halina Mwamuzi”
 Abdumalick Shaaban 

Kali Kitimoto mpiga kinanda wa Mashauzi

 Kimyaaaa!!! ndivyo wanavyomaanisha wadau hawa
 Mkurugenzi wa Jahazi Khamis Boha (kushoto) na Ally Jay
 Ilikuwa shangwe kila kona
 Saida Mashauzi akiimba Pendo la Ukakasi
 Saida Mashauzi
Nyomi
Isha akiimba mbele ya umati wa mashabiki
Waimbaji wa Mashauzi
Isha akikamilisha ratiba ya onyesho la miaka mitano ya Mashauzi

Comments

comments

About Saluti 5

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *