PJANIC AITAKA JUVENTUS IMWACHIE ASEPE ZAKE MANCHESTER CITY

MIRALEM Pjanic tayri ameonyesha azma ya kutaka kuondoka Juventus ili akatafute maisha mbele ya safari katika usajili huu dirisha la mwezi Januari.

Tena amekwenda mbali zaidi kwa kuitaja timu anayoipenda kwenda kukipiga na kwamba mapenzi yake ni kuvaa uzi wa Manchester City.

Kiungo huyo ameuomba uongozi wa klabu ya Juventus licha ya kumruhusu aondoke anataka kwenda kutimiza azma yake ya kucheza Ligi ya Premier.

Pjanic ambaye msimu huu amekuwa katika kiwango bora akiwa na Juve, ameweka bayana ndoto yake ya kucheza katika Ligi hiyo yenye mashabiki wengi.

“Nina malengo ya kutimiza ndoto ya kwenda kucheza katika Ligi ya premier.”

“Ninataka kuona ninalinda kipaji changu, sitaki kuwa msiri juu ya mimi kuondoka hapa.”

“Soka  ni kazi ninayokwenda kufanya kokote, ni mchezo wa kuangalia leo na kesho. Huu ndio msimamo wangu kwa sasa,” alisema Pjanic.


“Manchester City ni klabu ninayoipenda kwa ajili ya soka langu la baadae. Ninaamini nina nafasi ya kucheza nikiwa kule na kutimiza ndoto yangu hii.” 

No comments