PONDAMALI ‘AIKANA’ YANGA …asema hana mkataba Jangwani


KOCHA wa makipa ndani ya Yanga Juma Pondamali ameushangaza umma wa wapenda soka baada ya kusema hawezi kuzungumza lolote linalohusu mpira juu ya klabu hiyo kwa vile hana mkataba.

Akihojiwa na kipindi cha michezo cha radio Efm Jumamosi usiku, Pondamali alisema hana mkataba na Yanga.

Pondamali alitakiwa kutoa ufafanuzi juu ya tetesi kuwa haelewani na kocha mkuu George Lwandamina juu ya upangaji wa nafasi ya ugolikipa, lakini mlinda mlango huyo wa zamani wa Pan Africa, Yanga na timu ya taifa, akajibu kwa mkato na kukata simu.

“Mimi siwezi kuongelea mambo ya mpira Yanga kwasababu sina mkataba na Yanga,” alisema Pondamali na kukata simu.


Kwa majibu hayo, inaonyesha kuwa Pondamali yupo yupo tu Yanga na anafanya kazi kiholela bila mkataba wowote.

No comments