PSG YAINGIA VITANI NA JUVENTUS, TOTTENHAM KUWANIA SAINI YA KIUNGO EDUARDO SALVIO WA BENFICA

PARIS Saint – Germain wanapambana na timu za Juventus na Tottenham Hotspur wanaoongeza mbio za kuwania saini ya kiungo hodari wa klabu ya Benfica na Ureno, Eduardo Salvio.

Dalili za Salvio kutua katika kikosi cha mabingwa watetezi zinatiwa nguvu na taarifa kwamba kiwango chake kwa sasa kimewavutia baadhi ya mawakala wa klabu mbalimbali.

Wakitambua hilo, PSG wamemtengea kiungo huyo kitita cha pauni mil 22 wakiongeza dau waliloliweka awali ambalo lilikuwa pauni mil 15.

PSG walimsainisha kiungo huyo kuwa ni wa dau la mil 18 ingawa wameonyesha dalili za kukubali kushusha kiwango.

Benfica pamoja na kuweka bayana thamani ya mchezaji huyo, wamethibitisha kuwa Salvio ni miongoni mwa wachezaji wanaotakiwa na klabu mbalimbali za Ulaya.


“Ni kweli Salvio anawindwa na timu nyingi za Ulaya lakini tunataka acheze katika kikosi ambacho atapata namba ya kudumu. Ni mchezaji mwenye ofa nyingi ila ni jambo la kusubiri kuona ifikapo mwisho wa kipindi cha usajili,” ilieleza taarifa ya ndani ya Benfica.

No comments