RATIBA YA ‘WAATHIRIKA’ WA MOROGORO …FM WAKO MEEDA, JAHAZI EQUATOR, MSONDO BULYAGA, SIKINDE DDC KARIAKOO, MELODY, OGOPA KOPA MAPUMZIKO


BENDI sita kati ya saba kutoka Dar es Salaam zilizokuwa zishiriki tamasha la muziki wa taarab na dansi mjini Morogoro zimethibitisha kuwa hazitashiriki onyesho hilo.

Hiyo imefuatia kutolipwa malipo yaliyobakia na waandaaji (Tegemeo Arts) wa onyesho hilo lililopangwa kufanyika leo katika uwanja wa Jamhuri.

Bendi ambazo zimeitaarifu Saluti5 juu ya kujitoa kwao kwenye tamasha hilo ni FM Academia, Sikinde, Msondo, Jahazi Modern Taarab, East African Melody na Ogopa Kopa huku bendi pekee iliyowasili Morogoro ni Wakali Wao Modern Taradance.

FM Academia sasa watakuwa Meeda Club Sinza wakati Jahazi Modern Taarab watapatikana Equator Grill Mtoni huku Msondo Ngoma wakinguruma New Bulyaga Bar Temeke.

Sikinde sasa wataibukia kwenye uwanja wao wa nyumbani DDC Kariakoo, lakini East African Melody na Ogopa Kopa zenyewe zimetangaza kupumzika bila kufanya onyesho lolote.

Bendi hizo zimesema zimeathirika sana kwa ubabaishaji uliofanywa na waandaaji kwani wengine wamelazimika kuipitisha sikukuu kubwa kama ya X-Mas bila kazi huku wengine wakiandaa maonyesho ya kushtukiza.

No comments