REAL MADRID, BORRUSIA DORTMUND MECHI YA “HESHIMA” LEO

NI mechi kulinda heshima kati ya miamba miwili ya soka Hispania Real Madrid na Ujerumani Borrusia Dortmund.

Real Madrid itakuwa nyumbani kuwakaribisha vinara wa Kundi F Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Katika mchezo huo timu zote zimeshafuzu kwa hatua ya mtoano wa mashindano hayo na vita ndogo iliyobaki kati yao ni nani amemaliza wa kwanza.

Madrid wakiwa nafasi ya pili na pointi mbili nyuma watalazimika kushinda ili kumaliza wa kwanza dhidi ya Borrusia Dortmund yenye pointi 13 kileleni.

Hata hivyo bado sare itakuwa na maana kubwa kwa Dortmund kuendelea kubaki kileleni.

Katika mechi ya kwanza iliyochezwa Ujerumani wenyeji wa Dortmund walilazimika kusubiri hadi dakika za majeruhi kufunga bao la kusawazisha na kufanya matokeo kuwa 2-2.

Real Madrid itashuka dimbani ikiwa na rekodi nzuri ya kutopoteza mechi hata moja kati ya tano walizocheza dhidi ya Dortmund katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya wakishinda nne na sare moja.


Timu nyingine kwenye Kundi hilo Sportng CP na Legia Warsaw hazina nafasi na mechi yao ya mwisho ni kukamilisha ratiba.

No comments