REAL MADRID YAKATA NGEBE ZA BARCELONA CAMP NOU …Messi 0 Ronaldo 0, Sergio Ramos wee wacha tu


BARCELONA imenyamazishwa nyumbani kwao baada ya Real Madrid kulazimisha sare katika dakika ya mwisho.

Katika mchezo huo wa La Liga uliochezwa Camp Noun na kushuhudiwa mashabiki 90,000 huku uwanja mzima ukiwa umetapakaa rangi za Barcelona, Lionel Luis Suarez aliwapa raha mashabiki wake baada ya kuwafungia wenyeji bao la kuongoza dakika ya 53.

Kama ni mechi kati ya Messi na Ronaldo, basi hakukuwa na mbabe kati yao maana wote walitoka bila kuzifumania nyavu, lakini alikuwa ni beki Sergio Ramos aliyewanyamazisha wenyeji.

Wakati wengi wakianza kuamini kuwa Barcelona wanaondoka na ushindi, Ramos akafunga kwa kichwa dakika ya 90.

No comments