RIGOBERT SONG ASEMA MBWA WAKE NDIO ALIYEMNUSURU KUFA KWA KIHARUSI

BEKI wa zamani wa Liverpool na timu ya taifa ya Cameroon, Rigobert Song amesema mbwa wake ndie aliyemwokoa na kifo wakati aliposhikwa na kiharusi.

Song alishikwa na kiharusi na kupoteza fahamu hivi karibuni mjini Yaounde, Cameroon.

Hata hivyo Song ambaye pia ana mchango mkubwa kwa Cameroon kutamba Kombe la mataifa ya Afrika, alipona baada ya matibabu.

“Niliacha mlango wazi kwa sababu nilikuwa nasubiri mgeni. Sasa nikaanguka ingawa sikumeza ulimi na mbwa wangu aliponiona akaanza kubweka kwa nguvu,” alisema Song.


Song alisimulia kuwa kufuatia kelele za mbwa wake ndipo mwenyenyumba alipoenda kumuona na kuita gari la wagonjwa.

No comments