RIYAMA ALLY ASEMA HAHITAJI "KIKI", YEYE MWENYEWE NI KIKI TOSHA

NYOTA wa Bongomuvi Riyama Ally amesema kuwa misemo ya uswazi na kuvaa uhusika anapokuwa kazini ni kiki tosha ambazo zimemfanya awe matawi ya juu.

“Kwa jumla ni kwamba mimi mwenyewe ni kiki tosha kutokana na jinsi ninavyojiweka na ninavyokuwa wakati ninapoigiza hivyo vyote na vingine vingi muhimu vinatosha niendelee kujulikana zaidi,” alisema Riyama.

Alisema kwa heshima alizojiongezea katika tasnia ya filamu haitatokea hata siku moja akajiingiza kwenye mtandao wa kutumia kiki za aina yoyote ile kwa madai kwamba hazina nafasi kwake.


Riyama alisema kujituma na kuvaa uhalisia kwa msanii ndio nguzo ya kumfanya awe matawi ya juu lakini wale wasiojiamini ndiyo ambao wamekuwa wakijiongezea njia nyingine za kujifafutia umaarufu.

No comments