ROBERTO CARLOS ATAMANI KUFUNDISHA TIMU ZA LIGI KUU AUSTRALIA

NYOTA wa zamani wa Real Madrid na timu ya taifa ya Brazil, Roberto Carlos amesema kuwa anatamani kama angeweza kufundisha timu za Ligi Kuu ya Australia A – League.

Mkongwe huyo ambaye anasadikiwa kuwa beki bora katika historia ya soka na ambaye amewahi kutwa Kombe la Dunia mwaka 2002 akiwa na Brazil, hajawahi kupata kazi tangu mwaka jana alipoondoka kwenye timu inayoshiriki kwenye michuano ya Ligi ya India, Indian Super League, Delhi Dynamos.

Tangu aondoke katika timu hiyo, Roberto Carlos amekuwa akihusishwa kwenda ufundisha nchini Australia na huku mara kadhaa akiwa amezifundisha timu za Akhisar Belediyespor na Sivasspor za nchini Uturuki na ya Anzhi Makhachkala ya nchini Russia.


Wakati akiwa anafurahia kazi yake ya kuwa balozi wa vinara wa Ligi ya La Liga na ambao ni mabingwa wa Ulaya, Real Madrid, mkonge huyo mwenye umri wa miaka 43 ambaye amewahi kutwaa mataji matatu ya La Liga na idadi kama hiyo ya Ligi ya Mabingwa wakati akikipiga kwenye klabu ya jiji hilo kuu la Hispania, amesema kuwa angefurahi kama angefundisha Ligi hiyo ya Australia.

No comments