ROBERTO FIRMINO MATATANI KWA KUENDESHA GARI AKIWA AMEKUNYWA POMBE

STRAIKA wa Liverpool na timu ya taifa ya Brazil, Roberto Firmino amefunguliwa mashitaka kwa kunywa pombe na kisha kuendesha gari.

Kwa mujibu wa taarifa za vyombo vya habari, Firmino alikamatwa mapema mwishoni mwa wiki na polisi wa jiji la Liverpool na atafikishwa mahakamani Januari 31, mwakani.

Akizungumza juzi, msemaji wa polisi wa mji huo wa Merseyside aliuambia mtandao wa Liverpool Echo kuwa staa huyo alikamatwa mapema Jumamosi baada ya gari lake kusimamishwa na polisi katikati mwa mji huo.

“Polisi wa Merseyside wamemfungulia mashitaka mtu mwenye umri wa miaka 25 kwa kosa la kulewa na kisha akaendesha gari, baada ya kusimamishwa katikati ya mji wa Merseyside wa Liverpool mapema Jumamosi, Desema 24, mwaka huu,” alisema msemaji huyo.

“Roberto Firmino kutoka Liverpool atafikishwa mbele ya hakimu katika mahakama ya Liverpool City Januari 31, mwakani,” aliongeza msemaji huyo.


Liverpool watakutana na Chelsea katika mechi ya Ligi Kuu siku hiyo ambayo kesi inayomkabili Firmino itakuwa ikisikilizwa.

No comments