ROMA MKATOLIKI "AUMIA" WANIGERIA KULITAWALA SOKO LA MUZI BONGO

RAPA Roma Mkatoliki amefunguka na kusema kuwa huwa anaumia moyoni anapoona muziki wa Mnigeria unatamba nchini wakati wasanii wa Tanzania wapo na wana kazi nzuri.

Msanii huyo alisema kuwa amekuwa akijiuliza maswali mengi na hajui kama muziki wa nje kutamba nchini ina maana kwamba thamani ya wasanii imeshuka hapa nyumbani ama muziki wa nje ni muzuri kuliko wa Tanzania.

“Mimi kama msanii ninapata maswali kwanza inaniumiza ikidondoka ngoma ya Nigeria, yaani ndo habari ya mjini, mifano ndiyo hivyo (kwenye fainali ya shindano la Miss Tanzania) wanapigia maharusi wanapiga ngoma za nje,”alisema Roma.  

Rapa huyo alitoa ya moyoni katika kipindi  Planet Bongo cha EA Radio na kusema kuwa anashangazwa na kitendo cha mashabiki wa muziki nchini kupenda zaidi zaidi muziki wa nje kuliko ule wa wasanii wa nyumbani.

No comments