RONALDO ASEMA WACHEZAJI WENZIE REAL MADRID, URENO WANA MCHANGO MKUBWA TUZO YA BALLON D'OR

BAADA ya kutwaa tuzo yake ya nne ya Ballon d’Or, Cristiano Ronaldo ameeleza umuhimu wa wachezaji wenzake katika kupata heshima hiyo binafsi.

Wakati alikaa nje ya uwanja kwa muda mwingi wa mechi ya fainali ya Euro 2016, ulikuwa ni ubingwa wa timu ya taifa ya Ureno mjini Paris na Rewal Madrid kutwaa taji la 11 la Ligi ya Mabingwa ya Ulaya ambayo anaamini yamempa tuzo hiyo.

“Kwangu mimi ni heshima kubwa kutwaa Ballon d’Or yangu ya nne, hisia nilizonazo ni kama vile ndio tuzo yangu ya kwanza, ni ndoto iliyogeuka kuwa kweli tena. Sikuwahi kufikiria kuitwaa mara nne. Nina furaha sana,” alisema Ronaldo ambaye pia alishinda tuzo hiyo mwaka 2008, 2013 na 2014.

“Nachukua fursa hii kuwashukuru wachezaji wenzangu wote kuanzia kwenye timu ya taifa nay a Real Madrid, najivunia sana na nina furaha.”


“Bila ya Real Madrid au Ureno nisingetwaa tuzo hii hivyo daima naiweka timu yangu ya kwanza.”

No comments