RONALDO ATUMA SALAM ZA KRISMASI NA MWAKA MPYA KWA WATOTO WA NCHINI SYRIA WALIOKO KWENYE VITA YA WENYEWE KWA WENYEWE

MWANASOKA nyota duniani, Christiano Ronaldo ametuma salamu za Krismasi na Mwaka Mpya kwa watoto wa nchi ya Syria ambao wanaathirika kutokana na vita vya wenye kwa wenyewe.

Ronaldo ambaye ni balozi wa taasisi isiyokuwa ya kiserikali ya “Save Chiildren” aliwapa matumaini kuwa wawe na imani katika kipindi hiki kigumu.

“Pamoja na kuwa mii ni mwanasoka maarufu ninyi watoto wa Syria ndio mashujaa wa kweli. Dunia ipo pamoja nanyi,” alisema Ronaldo.


Nchi ya Syria imekuwa na wakati mgumu kutokana na vita ya wenyewe kwa wenyewe na mji wa Aleppo ndio umekuwa ukishambuwa zaidi.

No comments