Habari

SADIO MANE AWATOA HOFU MASHABIKI WA LIVERPOOL KUHUSU KUONDOKA KWAKE MWEZI JANUARI

on

MSHAMBULIAJI Sadio Mane amesisitiza kuwa Liverpool itaendelea kupigania ubingwa na kamwe haitapwaya  kwa kutokuwepo kwake. 
Sadio Mane atakosekana Liverpool kuanzia katikati ya mwezi Januari ambapo anajumuika na kikosi cha timu ya taifa cha Senegal kwenye michuano ya Kombe la Mataifa ya Africa (Africa Cup of Nations) itakayofayika nchini Gabon kuanzia Januari 14. 
Mshambuliaji huyo aliyenunuliwa kwa pauni milioni 30 kutoka Southampton, amekuwa muhimili mkubwa kwenye kikosi cha Jurgen Klopp na juzi aliifungia Liverpool bao pekee dhidi ya Everton na kuipeleka timu yake hadi nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya England.
Anaweza akakosa hadi mechi nane za Liverpool ikiwa ni pamoja na nusu fainali ya EFL Cup bila kusahau mtanange dhidi ya Chelsea utakaopigwa Januari 31. 
Likini mshambuliaji huyo amesema Liverpool ina hazina ya washambuliaji wenye vipaji na hivyo haoni kama kutakuwa na misukosuko yoyote ya kukosekana kwake.

Comments

comments

About Saluti 5

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *