SAMUEL ETO’O AMPA INIESTA TUZO YA MCHEZAJI BORA WA DUNIA

STAA Samuel Eto’o ni kama kampa tuzo ya mcheza bora wa dunia “Ballon d’Or” nyota Andres Iniesta baada ya kusema ndiye mchezaji bora kuliko Cristiano Ronaldo na Lionel Messi na huku akisema kuwa kiungo huyo ndie anayestahili kupewa tuzo hiyo.

Iniesta alirejea uwanjani Jumamosi wakati wa mechi ya El Clasico ambayo walitoka sare ya bao 1-1 dhidi ya Real Madrid ikiwa ni baada ya kukaa nje ya uwanja kwa muda wa mwezi mmoja na Eto’o anamuona mchezaji mwenzake huyo wa zamani wakiwa Barcelona ndiye mkali zaidi.

Wakiwa pamoja, wawili hao waliweza kutwaa ubingwa mara tatu wa michuano ya La Liga, mawili ya Ligi ya Mabingwa na Mcameroon huyo alimwagia sifa Iniesta alipoulizwa akimlinganisha na Messi na Ronaldo.

“Kwangu mimi Messi ni bora,” Eto’o aliuambia mtandao wa Telefoot. “Ni kama mwanangu kwangu nilimshuhudia wakati akija katika timu hii nzuri.


“Lakini nikimlinganisha na Iniesta, ulimwengu wa soka haumtendei haki kwani anastahili kupewa tuzo ya Ballon d’Or mara tatu ama nne, ni mchezaji mzuri vibaya mno,” aliongeza Eto’o.

No comments