SANCHEZ AZIDI KUIKOROGA ARSENAL, ASEMA HAVUTIWI NA MAISHA YA LONDON


WAKATI hatma ya Alexis Sanchez ndani ya Arsenal bado imezungukwa na ukungu, nyota huyo wa kimataifa wa Chile   amekiri kuwa maisha ya London hayamvutii. 

Sanchez aliyejiunga na Arsenal akitokea  Barcelona mwaka 2014 kwa ada ya pauni milioni 30 na kuibuka kuwa kipenzi cha mashabiki wa timu hiyo, mkataba wake unaisha mwaka 2018. 

Lakini mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 28 bado hajaamua iwapo atarefusha mkataba wake Emirates na tayari kuna ofa kutoka China itakayomwingizia pauni 400,000 kwa wiki. 

Sanchez amezidisha mashaka kwa mashabiki wa Arsenal baada ya kusema maisha ya London ni 'stress' tupu. 

Akizungumza na jarida la Arsenal, Sanchez alisema: "Natamani kutoka na kutembea sehemu kadhaa  na kula au kunywa na marafiki, lakini najionea kero na hivyo kuamua kubaki nyumbani. Jiji la London ndani ni kubwa na lina msongamano wa watu."

No comments